Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yakaribisha mchango wa Uchina katika kupambana na Ebola

Katika harakati za kuzuia maambukizi ya Ebola, WHO imepanga timu ya watu watakaofukua miili ya watu wanaohofiwa kufariki kutokana na maambukizi ya Ebola,kijiji cha Pendebu,Sierra Leone.Picha@WHO

WHO yakaribisha mchango wa Uchina katika kupambana na Ebola

Shirika la Afya Duniani, WHO, limekaribisha ahadi ya serikali ya Uchina ya kupeleka maabara ya kusafirishwa nchini Sierra Leone ili kusaidia kuongeza uwezo wa kupima kirusi cha Ebola nchini humo.

Mchango huo ni sehemu ya kuitikia ombi la WHO la usaidizi zaidi katika juhudi za kukabiliana na Ebola barani Afrika, na maombi ya serikali ya Sierra Leone.

Pamoja na wataalam wa maabara, timu ya watu 59 kutoka kituo cha udhibiti wa magonjwa nchini Uchina itwajumuisha pia watafiti wa magonjwa na wauguzi. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Margaret Chan amesema kuwa kinachohitajika kwa dharura zaidi na mara moja katika kukabiliana na Ebola ni wahudumu wa afya.