Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya tume ya mabadiliko ya tabianchi yazinduliwa New York

UN Photo/Mark Garten)
UN Photo/Mark Garten

Ripoti ya tume ya mabadiliko ya tabianchi yazinduliwa New York

Hapa New York, leo kumefanyika uzinduzi wa ripoti mpya kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya harakati zinazofanyika kuelekea mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wiki ijayo.

Ripoti imezinduliwa na mwenyekiti wa tume Felipe Calderon ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema athari ni dhahiri hivyo ni lazima kuchukua hatua ikiwemo matumizi ya nishati zisizochafua mazingira.

Harakati hizo zimefanyika huku nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zikiendelea na jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambapo miogoni mwao ni Tanzania ambako taasisi ya L's Solutions inasaidia watu wa kipato cha chini kutumia umeme utokanao na nishati ya jua na pia majiko yanayotumia kiasi kidogo cha kuni. Arnold Nzali ni mmiliki wa taasisi hiyo.

(Sauti ya Arnold)

Mkutano ya mwaka huu ni fursa ya kuwezesha kupatikana kwa makubaliano ya Kimataifa ya kukabiliana na athari za tabianchi mwakani