Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM, EU kuwanusuru wananchi wa CAR

Watu wakifanya kazi kufuatia mradi wa IOM na EU mjini Bangui.© IOM 2014

IOM, EU kuwanusuru wananchi wa CAR

Mashirika ya kimataifa yameanza kuchukua hatua za pamoja ili kukabiliana na hali mbaya inauoedelea kuwaandama wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na machafuko yanayoendelea.

Mashirika hayo lile la kimataifa linalohusika na wahamiaji IOM na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya yamekusanya nguvu ya pamoja kwa shabaha ya kuukwamua uchumi wa taifa hilo ambao unakaribia kabisa kuporomoka.

Makundi ya wakulima pamekuwa yakikusanywa ili kuendesha shughuli za uzalishaji mali zitakazowasaidia kuinuka kimaisha.

Chini ya mpango unaojulikana malipo kw akazi, jumla ya vikundi 750 kutokana makabila mbalimbali yameanza kutekeleza mpango huo ambao kwa sehemu ya kwanza unatekelezwa mjini mkuu Bangui.