Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR akutana na waathiriwa wa mgogoro Mali

Mkuu wa UNHCR akutana na waathiriwa wa mgogoro Mali

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR Antonio Guterres amefanya ziara nchini Mali na kufika mkoani Timbuktu amabako amekutana na mamalaka pamoja na wawakilishi wa asai za kiraia ambao wameathiriwa na mgogoro kaskazini mwa nchi hiyo. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(TAARIFA YA MSAMI)

Ni ndege ikiwasili uwanja wa ndege wa Timbuktu katika ziara iliyomkutanisha Mkuu huyu wa UNHCR na wenyeji jimboni hapa.

Bwana Guterres akatumia fursa hii kuitaka serikali ya Mali na vikundi vyenye saila kurejea katika meza ya mazungumzo na kuwaruhusu wakimbizi wa nchi hiyo walioko Niger, Burkina Faso na Mauritania kurejea nyumbani na kusisitiza..

(SAUTI GUTERRES)

"Tumeona kwamba raia wa Mali wanataka kurejea nyumbani lakini wanaona bado kuna magumu. Kwa hiyo tutashirikiana na serikali ya Mali, wananchi wa Mali, marafiki zetu na wadau wa Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuwezesha kuchangia kufikia amani, ustawi na maendeleo ambayo wananchi wa Mali wanastahili."

Kwa upande wake waziri wa mshikamano na ujenzi Kaskazini  mwa Mali Hamadoun Konaté amesema ataratibu usaidizi wa misaada ya kibanadamu ili kuleta ahueni kwa raia.

September mosi mwaka huu serikali ya Mali na wawakilishi wa vikundi vyenye silaha watakutana mjini Algiers, Algeria kufufua mazungumzo ya amani ambayo yalisitishwa.