Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuendelea kusaidia amani an maendeleo Somaliland

UN Photo/Eskinder Debebe)
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay,

UM kuendelea kusaidia amani an maendeleo Somaliland

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amewasili kwenye mji mkuu wa Somaliland, Hargeisa Jumatatu asubuhi na kusema umoja huo utaendelea na usaidizi wake kwenye eneo hilo.

Akizungumza mara baada ya kuwasili, Kay ambaye ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa Somalia, UNSOM amesema Somaliland imekuwa na maendeleo ya pekee na hivyo akatoa heko kwa serikali na wananchi wake.

Taarifa ya UNSOM imemkariri akieleza kuwa ziara hiyo itampatia fursa zaidi ya kuimarisha ushirikiano kati ya ujumbe huo na mamlaka za Somaliland kwa maslahi ya wananchi.

Akiwa Somaliland, Bwana Kay atakutana na viongozi waandamizi akiwemo Rais Ahmed Mohamed Mohamud Silanyo.