Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unene uliokithiri utotoni linazidi kuwa tatizo la afya duniani

Nembo ya WHO

Unene uliokithiri utotoni linazidi kuwa tatizo la afya duniani

Uzito wa kupindukia miongoni mwa watoto linakuwa tatizo la afya ya umma katika nchi nyingi zinazoendelea, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO.

WHO imesema idadi ya watoto wenye unene wa kupindukia kote duniani imeongezeka kutoka milioni 31 mwaka 1990 hadi milioni 44 wakati huu, huku nchi zinazoendelea zikishuhudia kiwango cha ongezeko kilicho asilimia 30 zaidi ya kile cha nchi zilizoendelea. Taarifa zaaidi na Amina Hassan

(Taarifa Amina)

Barani Afrika, takriban watoto milioni 10 wanaainishwakamawenye uzito uliokithiri.

Ilikukabiliana na tatizo hili sugu la unene uliokithiri miongoni mwa watoto, wiki hii WHO inafanya mkutano wa kwanza kabisa wa Kamisheni ya Kutokomeza Uzito Uliokithiri Utotoni. Dan Epstein kutoka WHO anaeleza zaidi.

“Kamisheni hii itachuguza hali zote zinazochangia unene wa kupindukia wa watoto wadogo. Hatua ya WHO ni kufuata mpango mathubuti wa kimataifa kuhusu mlo, mazoezi ya kimwili kwa ngazi za kimataifa, kikanda na hata mitaani. Sehemu ya hatua hiyo ni kamisheni hii-  inaangazia kila kinachohusiana na unene uliokithiri, kuanzia utangazaji wa vyakula vya watoto wachanga, njia za kuuzuia unene huo, kuupunguza katika watoto walioathiriwa tayari, na sera bora zinazoweza kuwekwa ili kuyafikia malengo haya."

WHO imesema watoto walio na uzito wa kupindukia wamo hatarini zaidi kubaki na uzito uliokithiri hata wakiwa wakubwa, na kupata magonjwa yasiyo ya kuambukizakamavile kisukari na magonjwa ya moyo katika umri mdodgo.

Ili kukabiliana na uzito uliokithiri, WHO inapendekeza mazoezi ya mwili mara kwa mara, kula matunda na mboga za majani zaidi, vitu kamamaharage, bidhaa za nafaka, na kupunguza matumizi ya mafuta na sukari.