Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaimarisha harakati dhidi ya Ukimwi Uganda

Makasha yaliyohifadhi kondomu ambazo IOM hutoa mgao nchini Uganda kama sehemu ya kudhibiti kuenea kwa HIV. (Picha @IOM Uganda)

IOM yaimarisha harakati dhidi ya Ukimwi Uganda

 

Nchini Uganda, Shirika la kimataifa linalohusika na uhamiaji IOM limeanzisha kampeni mpya ya kubadilisha tabia za watu kuhusu magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa kama njia ya kupambana na ukimwi nchini humo.

Msemaji wa IOM Christiane Berthiaume amesema sehemu zilizolengwa ni vijiji vya wavuvi na makazi ya wahamiaji wasio na vibali waliofukuzwa kutoka Tanzania, maeneo ya ziwaVictoria, ambapo zaidi ya asilimia 20 ya watu wameathirika na ukimwi.

Uhamasishaji wa IOM, kwa ushirikiano na serikali za mitaa nchiniUganda unalenga jamii iliyo kwenye mazingira magumu zaidi, kamamfano madereva, wavuvi, wahamiaji na makahaba, na kujaribu kuwaelimisha wahamishaji wenzao.

Zaidi ya waelimishaji 350 walifundishwa tangu mwanzo wa mradi mwaka jana, wakielewesha wenzao kuhusu ngono salama na utumiaji wa kondom.