Huko Hoima, Uganda nuru yarejea kwa watoto waliokabiliwa na ajira hatarishi
Wakati shirika la kazi duniani likiendeleza kampeni yake iitwayo Kadi nyekundu kwa wanaoajiri watoto kampeni iliyopigiwa chepuo zaidi tarehe 12 mwezi juni siku ya kupinga ajira za watoto duniani, nchini Uganda hususan wilaya ya Hoima, nuru inaanza kurejea kwa watoto ambao awali walikuwa hawaoni mwelekeo wa maisha. Je kulikoni? Basi John Kibego wa radio wahsirika Spice FM anaweka bayana kupitia makala hii.