Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu Cambodia kutathminiwa

UN Photo@Jean-Mac Ferr'e
UN Photo@Jean-Mac Ferr'e

Haki za binadamu Cambodia kutathminiwa

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Cambodia, Surya P. Subedi atafanya ziara ya  siku 10 kutoka tarehe 15 hadi 25 Juni nchini humo, ikiwa ziara yake ya 11 katika nchi hiyo, ili kujifahamisha maendeleo yaliyotekelezwa kufikia sasa kwa ajili ya makubaliano ya hapo awali,  hasa yale yanayohusu sheria, bunge, marekebisho ya uchaguzi na umiliki wa ardhi.

Mtaalam huyo atakutana na wakuu wa serikali, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika wa kiraia, pamoja na wanabiashara ili  kujifahamisha zaidi yanayojiri nchiniCambodia.

Bwana Subedi ana jukumu la kuwasilisha ripoti yake kila mwaka kwa Baraza la Haki za Binadamu tangu kuteuliwa kama Mtaalam Maalum anayeshughulikia haki za binadamu nchiniCambodia, na anatarijiwa kuwasilisha ripoti yake mwezi Septemba mwaka huu.