Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaimarisha operesheni zake Sudan Kusini

usambazaji wa chakula na FAO pamoja na WFP @FAO

FAO yaimarisha operesheni zake Sudan Kusini

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO imetilia mkazo zaidi operesheni zake za kufikisha msaada wa dharura katika sehemu nyingi zilizokumbwa na vita nchini Sudan Kusini. Taarifa zaidi na John Ronoh.

(Taarifa ya John)

Uimarishaji wa operesheni hizo unahusisha FAO kuongeza muda wa  usaidizi wa dharura kwa miezi mitatu zaidi ili kufikia wakulima, wavuvi  pamoja na wafugaji walioathiriwa na vita.

Imesema inatekeleza hayo licha ya matatizo ya kufikia maeneo husika pamoja na kuzorota kwa usalama katika sehemu nyingi nchini humo.

Tangu kuanza kwa mapigano Sudan Kusini, FAO imetoa zaidi ya vifaa vya misaada Laki Moja zikiwemo mbegu za mazao, vifaa vya uvuvi na dawa za mifugo kwa minajili ya kuokoa maisha ya waathairiwa hao.

Ikiwa na msaada wa dola Milioni 42, FAO imeweza kusaidia watu milioni 1.3, lakini kuna umuhimu wa msaada zaidi ili kuwezesha Shirika hilo kufikia sehemu nyingine ambazo zimekumbwa zaidi na upungufu wa chakula.