Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutekwa kwa wasichana Nigeria, Mwakilishi wa Ban aanza ziara ya pili

Said Djinnit, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UM na Mkuu wa ofisi ya UM huko Afrika Magharibi. (Picha@UN/JC McIlwaine)

Kutekwa kwa wasichana Nigeria, Mwakilishi wa Ban aanza ziara ya pili

Tukielekea Afrika hii leo, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Afrika Magharibi, Said Djinnit, ameanza ziara yake ya pili nchiniNigeriakuangalia jinsi gani Umoja wa Mataifa unaweza kusaidia serikali kurejesha wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara huko Chibok tarehe 14 mwezi uliopita.

Djinnit atakuwa na mashauriano na wadau mbali mbali pamoja na watendaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchiniNigeria, katika shughuli yake ya kutimiza mpango jumuishi wa kusaidiaNigeria.

Katika ziara yake ya kwanza, kwanzia tarehe 12 hadi 15 Mei, alijadili na viongozi waNigeriakuhusu mchango wa Umoja wa Mataifa katika juhudi za kuwasaka na kuhakikisha wasichana hao wanaachiliwa huru wakiwa salama.