Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi halali Afghanistan ni muhimu kusitisha umwagaji damu:UNAMA

Jan Kubis akiongea juu ya duru ya pili wa uchaguzi wa rais-Afghanistan@UNmultimedia

Uchaguzi halali Afghanistan ni muhimu kusitisha umwagaji damu:UNAMA

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Afghanistan Ján Kubiš amesihi vyombo vyote vinavyohusika na duru ya pili ya uchaguzi wa urais  nchini humo pamoja na wagombea waheshimu makubaliano ya pamoja ili kulinda uhalali wa matokeo ya uchaguzi huo.

Bwana kubis ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA amesema hayo huko Brussells mji mkuu wa Ubelgiji wakati wa mkutano ulioandaliwa na Umoja wa kujihami wa nchi za magharibi, NATO ukihusisha mawaziri wa ulinzi kutoka nchi zinazochangia jeshi la msaada la kimataifa ISAF.

Amesihi nchi zote ziendele kusaidiaAfghanistanna majeshi yake ili kuwe na usalama zaidi.

Huku akitambua kuimarika kwa mchakato wa uchaguzi kama ilivyoshuhudiwa tarehe Tano Aprili, Kubis amesemaAfghanistaniko katika kipindi muhimu na maboresho zaidi kwenye uchaguzi, yanahitajika.

Amesema wagombea wawili wa kiti cha Urais wanataka maboresho zaidi kwenye mchakato wa uchaguzi na kile muhimu ni kwamba vyombo vya uchaguzi vinaonekana kutekeleza majukumuyaokwa nia njema; hivyo basi amevisihi viendelee kuhakikisha uwazi kwenye uamuzi wao, na matendoyao.