Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Abyei, Somalia na Guinea Bissau zaongezewa muda

UN Photos
Baraza la Usalama likipiga kura. @

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Abyei, Somalia na Guinea Bissau zaongezewa muda

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepitisha maazimio matatu ya kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye maeneo ya Abyei, nchini Somalia na Guinea Bissau.  Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte

Rais wa Baraza hilo, ambaye ni Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Korea, Oh Joon, amesema:

“ Matokeo ya kura ni yafuatavyo. Azimio la jaribio limepata kura 15. Azimio hilo limepitishwa kwa kauli moja, kama azimio nambari 2156” 

Kuhusu Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Abyei, UNISFA, Baraza la Usalama limekiri kusitikitshwa na kwamba nchi za Sudan na Sudan Kusini zimeshindwa kupata maelewano kuhusu maeneo hayo yanayopakana nchi hizo mbili.

Ujumbe wa UNIOGBIS- Guinea Bissau, umeongezwa muda wake kwa kipindi cha miezi sita, azimio la Baraza la Usalama likikaribisha vyema mafanikio katika kuandaa uchaguzi wa raisi na wa bunge hivi, lakini pia likieleza wasiwasi wake juu ya hali ya uharibifu na utumikishwaji wa rasilimali hivi karibuni.

Hatimaye, Baraza la Usalama limeongeza muda wa UNSOM, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa  huko Somalia, kwa mwaka moja, likisisitiza umuhimu wa kutunza haki za binadamu na kupambana na ukatili dhidi ya wanawake, na kutayarisha uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwaka 2016.