Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maadhimisho ya miaka 25 ya CRC kufanyika tarehe 20 mwezi Novemba

UN Photo/Evan Schneider
@

Maadhimisho ya miaka 25 ya CRC kufanyika tarehe 20 mwezi Novemba

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limepitisha azimio la mwelekeo wa maadhimisho ya miaka mitano tangu kuridhiwa kwa mkataba wa haki za mtoto duniani, CRC.

Wajumbe walipitisha azimio namba A/68/L.46 linalotangaza rasmi kuwa tarehe 20 mwezi Novemba mwaka huu itakuwa maadhimisho rasmi ya mkataba huo wenye misingi mikuu minne ya haki za mtoto ambazo ni Kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa.

Siku hiyo kutakuwa na mikutano miwili ya ngazi ya juu ukiangazia utekelezaji wa haki za mtoto hususan kwenye mizozo na hata majumbani.