Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuondoe vikwazo vya soko la dawa tuokoe maisha:UNITAID

Picha ya UNITAID

Tuondoe vikwazo vya soko la dawa tuokoe maisha:UNITAID

Ripoti ya mwaka ya Ushirikiano wa kimataifa wa kuwezesha upatikanaji wa dawa dhidi ya Kifua Kikuu, Malaria na Ukimwi, UNITAID imepigia chepuo hatua zinazochukuliwa na ushirikiano huo za kuondoa vikwazo kwenye soko la dawa ili kuokoa mamilioni ya watu wanaohitaji tiba dhidi ya magonjwa hayo. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

(Taarifa ya Alice)

Ripoti ya mwaka ya UNITAID inasema tiba mahsusi na vifaa vya uchunguzi dhidi ya Malaria, Kifua kikuu na HIV/AIDS vinaibuka sasa ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya miongo kadhaa, lakini kuna vikwazo katika soko vinavyopaswa kuondolewa ili huduma hizo ziwafikie mamilioni ya wakazi wa nchi za vipato vya kati na chini.

Ripoti hiyo iitwayo Kurekebisha masoko ili kuokoa maisha, inataja vikwazo hivyo kuwa ni pamoja na bei za juu , hataza na ukosefu wa mifumo inayowezesha upatikanaji tiba na vifaa tiba kulingana na mazingira husika.

UNITAID imetoa ripoti hiyo wakati ambapo mwezi huu tarehe Sita iliingiza dola Milioni 160 katika soko ili kuwezesha wananchi maskini kupata tiba dhidi ya homa ya ini, Hepatitis-C na kifua kikuu sugu. Dkt. Phillipe Duneton ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNITAID.

(Sauti ya Dkt.Duneton)

UNITAID ilianzishwa mwaka 2006 na serikali za Brazil, Chile, Ufaransa, Norway na Uingereza, hata hivyo hivi sasa imepanua wigo wake na kujumuisha Cyprus, Jamhuri ya Korea, Luxembourg, Hispania na Tasisi ya Bill na Melinda Gates. Nchi nyingine niCameroon,Congo,Guinea,Madagascar,Mali,MauritiusnaNiger.