Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Milioni Tatu waweze epushwa na vifo kila mwaka: UNICEF

Mama akiwa amembeba mwanae kwa njia ya Kangaroo ili kumpatia joto.(Picha-Maktaba)

Watoto Milioni Tatu waweze epushwa na vifo kila mwaka: UNICEF

Ripoti za aina yake kuhusu hatua za kulinda uhai wa watoto duniani zimetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake zikieleza kuwa uhai wa watoto Milioni Tatu ulimwenguni ambao hufariki dunia kabla ya kutimiza umri wa mwaka mmoja unaweza kuepushwa iwapo watapata huduma stahili pindi tu wanapozaliwa.

UNICEF na wadau wake kwenye machapisho ya Lancet wametaja mbinu hizo kuwa ni pamoja na kunyonya titi la mama, kupatiwa usaidizi wa kupumua na hata kutumia mbinu ya kangaroo ya mama kumbeba mwanae kifuani hususan kwa watoto njiti.

Dkt. Mickey Chppra mkuu wa mipango ya afya ya dunia kwenye WHO amesema kipindi cha toka mama anapata uchungu hadi saa za awali baada ya mtoto kuzaliwa ni kipindi muhimu zaidi kwa mustakhbali wa mtoto anayezaliwa na mama yake kwani karibu nusu ya vifo vya uzazi hutokea ndani ya saa 24 baada ya mtoto kuzaliwa.

UNICEF imetaja nchi kama vile Rwanda ambayo imepata maendeleo katika kuokoa uhai wa mama na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano wakati huu ambapo idadi kubwa zaidi ya vifo vya watoto wachanga imetajwa kuwa ni kwenye nchi za Kusin mashariki mwa Asia ikifuatia na nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara.

Mfululizo wa machapisho ya Lancet huandaliwa na wataalamu kutoka UNICEF, shule ya sayansi na magonwja ya kitropiki ya London na chuo kikuu cha Agakhan.