Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola Bilioni 150 zapatikana kwenye ajira haramu: ILO

UN Photos
@

Dola Bilioni 150 zapatikana kwenye ajira haramu: ILO

Shirika la kazi duniani, ILO limesema utumikishaji kwenye sekta binafsi umesababisha faida haramu ya dola zaidi ya Bilioni 150 kwa mwaka, ikiwa ni mara tatu zaidi ya kiwango kilichokadiriwa. Ripoti ya Priscilla Lecomte inafafanua zaidi.

(Ripoti ya Priscilla)

Kwa mujibu wa ripoti ya ILO, theluthi mbili za pesa hizo zinatokana na utumikishaji wa kingono, wanawake wa wasichana wakiwa hatarini zaidi ya kutumikishwa. Kwa jumla, zaidi ya watu milioni 21 wanajihusisha na shughuli hizo, hasa katika sekta binafsi, na zaidi katika ukanda wa Asia-Pacifiki.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani, Guy Rider, amepongeza bidii za serikali kupunguza ajira haramu serikalini, na kuimarisha takwimu zao lakini pia amewaomba waendelee kupambana na vyanzo vya ajira hizo haramu kama vile umaskini, ukosefu wa elimu na ustawi wa jamii, au uhamiaji haramu huku akisema..

(Sauti ya Rider)

"Iwapo tunataka kuleta mabadiliko ya dhati katika maisha ya wanawake, wanaume na watoto Milioni 21 ambao bado wanatumikishwa kwenye ajira, tunahitaji kucukua hatua za haraka. Kuendelea kuwepo kwa utumikishaji wa binadamu ni mbaya kwa wanaotumikishwa na kwa maendeleo pia. Ni tabia ambayo haina fursa katika jamii ya sasa. Ni wakati wa kushirikiana na kutokomeza kabisa sekta hii yenye faida lakini wakati huo huo chanzo cha jambo baya na la aibu.”