Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WTO yaonya dhidi ya utumikishwaji wa watoto katika sekta ya utalii

@UNICEF Tanzania

WTO yaonya dhidi ya utumikishwaji wa watoto katika sekta ya utalii

Shirika la Kimataifa la Utalii WTO limesaini makubaliano na ofisi ya World Vision ya Ukanda wa Asia ya Kusini-Mashariki ili kutokomeza utumikishwaji wa watoto katika sekta ya utalii.

Makubaliano hayo yanalenga kuwezesha mbinu na tabia nzuri ya kulinda watoto, kupitia kampeni iitwayo Utalii salama kwa watoto inayoongozwa na World Vision kwa ufadhili wa serikali za Cambodia, Laos, Vietnam na Thailand, ili kuelimisha watalii dhidi ya unyanyasaji wa watoto.

Katibu Mtendaji wa WTO, Taleb Rifai, amesema, ukuaji wa utalii ni fursa kwa maendeleo lakini pia ni changamoto kubwa hasa kwa watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, na kwamba watoto na vijana wako hatarini zaidi.

Ameongeza kuwa ni lazima wadau mbalimbali washirikiane ili kupambana na shida hiyo kubwa ya utumikishwaji wa watoto.

Kwa miaka 15 sasa WTO inaongoza mtandao wa kimataifa wa kulinda watoto katika sekta ya utalii.