Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miezi sita baada ya kimbunga Haiyan mahitaji kurejelea hali ya awali bado ni mengi

Waathirika wa kimbunga Haiyan (picha ya maktaba)

Miezi sita baada ya kimbunga Haiyan mahitaji kurejelea hali ya awali bado ni mengi

Hali ngumu bado inaendelea kuwaandaama mamia wa raia wa Philipine ambao makazi yao yaliharibiwa na kipunga Haivan kilichoipiga nchi hiyo miezi sita iliyopita.

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu pamoja na lile la hilali nyekundu yamezindua mpango mpya wenye shabaha ya utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa raia hao ambao habado wanataabika

Taarifa kamili na George Njogopa

(TAARIFA YA GEORGE)

 Zaidi ya watu milioni 16 waliathiriwa na kimbunga hicho huku mamia kadhaa wakipoteza ngudu na jamaa zao. Pia eneohilolilikumbwa na uharibifu mkubwa ikiwemo kusombwa kwa nyumba kadhaa na maeneo mengine yakishuhudia uharibifu wamalina mioundo mbinu.

Wakati eneo la mashariki mwa Visayas, likitajwa kuwa na uhitaji mkubwa pia kuna ripoti kuwa watu wanaoishi maeneo ya mbali wapo katika hali mbaya na wanahitaji usaidizi wa haraka.

Mashirika ya utoaji misaada ya usamaria yameanzisha juhudi za usambazaji wa misaada na kwamba misaada ya awali imelenga kuwasaidia zaidi ya watu 775,000 .

Tangu eneohilolikumbwe na kimbunga miezi sita iliyopita, ni mashirika machache tu ya usamaria mwema yamekuwa yakisambaza huduma kwa waathirika hao hali inayofanywa wengi wao kuendelea kwenye uhitaji mkubwa.