Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutopatikana takwimu sahihi kikwazo katika mapambano dhidi ya malariaTanzania

Kutopatikana takwimu sahihi kikwazo katika mapambano dhidi ya malariaTanzania

Wakati siku ya kimataifa ya malaria ikiadhimishwa hii leo takwimu za kitaifa nchini Tanzania zinaonyesha kupungua kwa asilimia nane kwa ugonjwa huo licha ya kwamba kwa baadhi ya maeneo nchini humo  ukosefu wa takwimu sahihi unaotokana na wagonjwa wengi kutopata tiba sahihi ni moja ya changamoto.

Katika mahojiano na idhaa hii mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Ryvuma Benedcito Ngaiza anasema licha ya kwamba mkoani humo tatizo la malaria linaonekana kukuwa lakini bado takwimu hizo zina mapungufu.

(SAUTI BENEDICT)

Kadhalika mganga huyo mfawidhi anaeleza mikakati ya kupambana na malaria.

(SAUTI BENEDICTO )