Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya mama dunia, wito wa kujali sayari hii kwamanufaa ya binadamu watolewa

Leo ni siku ya mama dunia, wito wa kujali sayari hii kwamanufaa ya binadamu watolewa

Leo ni siku ya mama dunia ambapo umuhimu wa sayarui dunia unaangaziwa. Katika kuadhimisha siku hii Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, John William Ashe, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchagiza maendeleo endelevu na matumizi ya vyanzo vya nishati mbadala katika miji na vijijini. Taarifa kamili na Joseph Msami

(TAARIFA YA MSAMI)

Katika ujumbe wake wakati wa mjadala kuhusu siku hii adhimu Bwana Ashe anasisitiza juu ya uelewa wa watu juu ya masuala ya mazingira na kiuchumi na anasema

(SAUTI ASHE)

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya dunia ya kisayansi na taaluma ya makataba kuhusu makubaliano ya hali ya hewa Dk Richard Muyungi ametaka binadamu wanoishi katika sayari dunia kutatua ongezeko la gesi joto akisema huo ndiyo muarubaini pekee wa kunusuru sayari hii

(SAUTI DK MUYUNGI)