Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgao wa chakula kwa wakimbizi Uganda sasa ni asilimia 100: WFP

Mgao wa chakula kwa wakimbizi Uganda sasa ni asilimia 100: WFP

Wakimbizi wote nchini Uganda wameanza kupokea msaada wa chakula wa asilimia mia moja kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), baada ya msaada huo kukatwa mwanzoni mwa mwaka huu kutokana na uhaba wa fedha. John Kibego wa radio washirika ya Spice FM nchini Uganda na melezo kamili

(TARIFA YA JOHN KIBEGO)

Shirika la WFP lililazimika kukata msaada wa chakula kwa asilimia hamsini kwa wakimbizi wote waliofika Uganda kabla ya Oktoba mwaka jana, ili kuwapa kipao mbbele wakimbizi wapya waliokuwa wakimiminika kutoka Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)

Hatua hiyo iliathiri wakimbizi katika kambi zote tisa na vituo vitano vya kupokea wakimbizi humo nchini .

Lydia Wamala Msemaji wa WFP hapa Uganda anasema walichukua uamuzi huo mgumu kwa sababu za ufadhili mdogo uliokuwa ukipatikana.

(Sauti ya Lydia Wamala)

Mkimbizi hapa Uganda hupewa kipande cha ardhi kuwawezesha kujishughulisha kwa klimo, na khukubaliwa kufanya biashara kwa sababu za ustawi, kando ya kupata misaada kutoka mashirika mbali mbali.