Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uelewa kuhusu usonji bado mdogo, wenye usonji huitwa vichaa:

Uelewa kuhusu usonji bado mdogo, wenye usonji huitwa vichaa:

Fikra potofu na imani za kishirikina ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kukwamisha juhudi za kitabibu za kuokoa watoto wenye usonji au ulemavu wa akili nchini Tanzania.

Ni kauli aliyotoa Brenda Shuma, Mkurugenzi wa Kituo cha Gabriella kilichoko mkoani Kilimanjaro alipozungumza na idhaa hii leo siku ambayo ni ya kimataifa ya kuhamasisha elimu juu ya ulemavu wa akili au usonji.

(Sauti ya Brenda)

Grace Lyimo mzazi wa mtoto mwenye usonji na anaeleza kilichomkuta alipokwenda kwa daktari kupata suluhu ya mwanae.

(Sauti ya Grace)

Kituo cha Gabriella mjini Moshi, hupokea watoto wenye usonji na kuwapatia stadi wao na wazazi wao ya kuwawezesha kujumuika katika jamii na jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda. Mahojiano kamili yatapatikana kwenye ukurasa wetu.