Watu zaidi wafariki Guinea kutokana na mlipuko wa Ebola

28 Machi 2014

Shirika la Afya Duniani, WHO, limetangaza leo kwamba tayari watu 66 wamefariki kutokana na virusi vya Ebola, mwezi mmoja tu baada ya kuibuka kwa virusi hivyo nchi Guinea, Afrika ya Magharibi. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte

(Taarifa ya Priscilla)

Hadi leo, Shirika la Afya, WHO, limebaini visa 103 vinavyoshukiwa kuwa vya virusi vya Ebola, katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Guinea, lakini bado wataalamu wa afya hawajathibitisha kuwa visa vyote ni vya Ebola. Lakini tayari shirika la WHO limeshuhudia kwamba watu 66 wamefariki kutokana na ugonjwa huu. Visa vyote vimeasiliwa na eneo moja la Guinea.

Mtaalam wa WHO Gregory Hartl amesema kwamba ubaya wa homa hiyo hatari ni kutokuwa na matibabu wala chanjo, na wanaoathirika na ugonjwa huo wanaumwa sana, hadi kufa kwa asimilia kubwa.

Amesisitiza kwamba, ingawa ugonjwa huo ni mbaya na huambukiza kwa kasi, ni muhimu kutoogopa zaidi wala kubagua wagongjwa. Hivi sasa mashirika yasiyo ya kiserikali yamegundua kwamba wagonjwa wengine wanajificha na kuogopa kwenda kutibiwa, hali ambayo inawazuia wataalam wa afya kupambana vyema na ugonjwa huo.

Sauti ya Gregory ………

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud