Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa EXPAND-TB waleta nuru katika vita dhidi ya Kifua Kikuu Tanzania: Dkt. Mleoh

Mradi wa EXPAND-TB waleta nuru katika vita dhidi ya Kifua Kikuu Tanzania: Dkt. Mleoh

Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya Kifua Kikuu duniani tarehe 24 mwezi huu, nchini Tanzania harakati za kupambana na ugonjwa huo ikiwemo Kifua Kikuu sugu zinaanza kuzaa matunda. Nuru hiyo inatokana na mradi wa shirika la afya duniani, WHO unaolenga nchi 27 ikiwemo Tanzania ambako Kifua Kikuu Sugu kinahatarisha afya ya umma. Je mradi huo umefanya nini? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza kwa njia ya simu na Dokta Liberate Mleoh, Naibu Meneja wa Mradi wa Kitaifa wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini humo ambaye anaanza kwa kuelezea hali ya ugonjwa huo Tanzania.