Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unesco yalaani mauaji ya wanahabari wawili Syria

Unesco yalaani mauaji ya wanahabari wawili Syria

Mkurugenzi mkuu wa shirika la  Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO, Irina Bokova amelaani mauaji ya waandishi wawili nchini Syria Abdul Quader na Ali Mostafa na kurejelea umuhimu wa watu kupata taarifa kama sehemu ya kutatua mgogoro.

Bi Bokova ametaka pande zote nchiniSyriakusaidia waandishi wa habari katika kutimiza majukumuyaokuripoti katika mazingira magumu huku pia akitaka majina ya wanahabari hao yaongezwe katika orodha ndefu ya raia  wahanga wa machafuko.

Omari Qader aliyekuwa na umri wa miaka 27 ambaye alikuwa mpiga picha wa televisheni ya Beiruti katika kituo kiitwacho Al- Mayedeen aliuawa Machi 8 wakati akiwa kazini kuripoti machafuko mashariki mwa nchi katika jimbo liitwalo Deir Al-Zour.

Kwa upande wake mwandishi wa kujitegemea kutoka Canada Ali Moustafa, aliyekuwa ana umri wa miaka 29 aliuawa siku inayofuatia akiwa ni miongoni mwa watu Wanane waliokufa baada ya mlipuko wa bomu mjiniAleppo.

Vifo vya wanataaluma hao wawili vinafikisha idadi ya wanahabari watano ambao mauaji yaonchini Syriayamelaaniwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO.