Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM walaani kifo cha mwanaharakati China

Wataalamu wa UM walaani kifo cha mwanaharakati China

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limeeleza hofu yake juu ya kifo cha mwanahakarati Cao Sun Ly Shunli kilichotokea hospitali huko China tarehe 14 mwezi huu huku wakituma rambirambi kwa familia yake na marafiki.

Wataalamu hao wamesema hayo katika ombi lao kufuatia kifo chake huku wakisema taarifa za Bi. Cao mwanasheria maarufu wa masuala ya haki za binadamu nchini China za kupotea, kushikiliwa kizuizini na kunyimwa matibabu ziliwasilishwa kwao na wao kuwasilisha ombi la dharura kwa China ili ahudumiwe.

Wataalamu hao wametaka serikali ya China ichunguze haraka mazingira ya kifo chake wakisema tukio hilo ni mfano wa kuharamisha harakati za watetezi wa haki za binadamu nchini China na halikubaliki.

Bi. Cao alitoweka mwezi Septemba mwaka jana baada ya kuzuiwa na mamlaka za China kupanda ndege kwenda Geneva kushiriki mchakato wa tathmini ya pili ya haki za binadamu nchini mwake.

Hakujulikana alipo hadi aliposhtakiwa kwa uhalifu wa uchochezi. Hali yake ya kiafya ilizorota akiwa kizuizini na alihamishiwa hospitalini akiwa katiak hali mbaya mwezi uliopita