Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa UM ataka kusiwepo visingizio vya siri za kitaifa kufanya utesaji

Mtaalam wa UM ataka kusiwepo visingizio vya siri za kitaifa kufanya utesaji

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu utesaji, Juan Mendez, ameshutumu utesaji wa watu kwa kisingizio cha kile kinachoitwa siri ya taifa, akisisitiza kuwa ukiukwaji huo wa haki za binadamu usikubalike kwa misingi yoyote.

Akilihutubia Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Bwana Mendez ameonya kuwa kila wakati mtu anapotoa ushahidi wa siri katika mahakama, kuna uwezekano wa hatari ya sehemu ya ushahidi huo kupatikana kupitia uteseaji au uovu mwingine, kwani ushahidi kama huo hauwezi kuchanganuliwa mahakamani.

Ameongeza kuwa tangu vita dhidi ya ugaidi vilipoanza, mataifa mengi hukataa kuruhusu kazi za vyombo vya ujasusi na usalama kukaguliwa au kuchunguzwa na taasisi za kimataifa.