Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya kisasa kurahisisha ukusanyaji wa takwimu: Tanzania

Teknolojia ya kisasa kurahisisha ukusanyaji wa takwimu: Tanzania

Wakati mkutano wa 45 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Takwimu unaendelea mjini New York Marekani kuangalia jukumu la takwimu katika ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015,Tanzania imesema wakati umefika kuungana na mataifa mengine katika kutumia teknolojia za kisasa kukusanya takwimu ili kuhakikisha mfumo utumikao unaendana na ule ya kimataifa.

Dkt Albina Chuwa anayewakilishaTanzaniakwenye mkutano huo ameiambia Idhaa hii katika mahojiano maalum kwambahiloni muhimu kwani kwa sasa takwimu zinatakiwa kukusanywa kila wakati na si kusubiri baada ya miaka miwili..

(Sauti ya Dkt Chuwa)

Naye Kamishna wa sensaTanzaniamwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said ametaja jambo muhimu la kuzingatia ili takwimu iweze kuchangia kwenye maendeleo.

 (Sauti  ya Hajjat Amina Mrisho Said)

Mahojiano kamili kati ya Hajjat Amina na Dokta Chuwa yanapatikana kwenye tovuti yetu.