Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti mpya ya UM yamulika ukiukwaji wa haki za binadamu Uganda`

Ripoti mpya ya UM yamulika ukiukwaji wa haki za binadamu Uganda`

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa ripoti mpya kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Uganda. Ripoti hiyo inatia mstari wa mbele taasisi ya polisi ikifuatwa na jeshi la serikali ya nchi hiyo. Hi hapa ni tarifa kamili na John Kibego wa radio washirika ya Spice FM nchini humo.

(Taarifa ya John Kibego)

Ripoti hii iliyotolewa jijini Kampala inasema, vyombo vya usalama ndivyo vinaongoza katika kukiuka haki za binadamu. Kati ya malalamiko 590 yaliopokewa na ofiti hiyo dhidi ya vyombo vya usalama kuanzia mwezi Januari mwaka 2012 hadi Septemba 2013, polisi waliongoza na visa 287.

Inaendela mbele kufichua kwamba, jeshi la serikali la UPDF na kitengo chake cha intelijensia wa kijeshi (CMI), wanashikilia nafasi ya pili wakifuatwa na askari wa magereza.

Vyombo hivyo vilikiuka haki za binadamu kwa njia tofauti zikiwemo utesaji, kuwazuia washukiwa bila kuwapeleka mahakamani, kusikiliza kesi za raia washuliwa katika mahakama ya kijeshi na kukandamiza haki ya watu kukusanyika na kujieleza.

Ofisi hiyo ya haki ya Umoja wa Mataifa ilisajili jumla ya malalamiko 909 yakiwemo hayo dhidi ya vyombo vya usalama.