Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yachukua hatua za dharura za mahitaji ya wajawazito Ufilipino

UNFPA yachukua hatua za dharura za mahitaji ya wajawazito Ufilipino

Shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA limeungana na tamko la Umoja huo la kutangaza kiwango cha juu zaidi cha dharura nchini Ufilipino kufuatia janga la kimbunga Haiyan zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

Mkurugenzi Mkuu wa UNFPA Dkt. Babatunde Osotimehin amesema hali hiyo imefanya wapatie kipaumbele cha juu huduma zake eneo hilo hususan zile za afya ya uzazi kwa mamilioni ya wanawake na wasichana ikiwemo vifaa salama vya kujifungua, huduma za dharura kwa watoto wachanga.

Amesema yakadiriwa wajawazito Laki Moja na Themainini watahitaji huduma za dharura za uzazi ingawa maeneo mengi yaliyoathiriwa na kimbunga hicho bado hayafikiki.