Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaonya machafuko kuongezeka CAR

UNHCR yaonya machafuko kuongezeka CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR linasema hali inazidi kuwa mbaya katika mji mkuu wa jamahuri ya Afrika ya Kati, CAR, Bangui ambapo mauaji yanendelea.

UNHCR inasema kuna ukatili wa wazi unaofanywa zaidi na waasi huku pia ikionya kuwa bunge la nchi hiyo limetoa matamko yanayoweza kuchochea vurugu. Idadi kubwa ya waisilamu inaripotiwa kukimbia ili kujinusuru huku kukiwa na taarifa ya ya makundi ya watu kuwasaka watu wa dini tofauti wakati huu ambapo kiwango cha chuki kinarpotiwa kuwa juu.

Rupert Colville ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI RUPERT)