Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunyima watu chakula, maji, malazi na huduma za afya vyatumika kama mbinu ya vita Syria:

Kunyima watu chakula, maji, malazi na huduma za afya vyatumika kama mbinu ya vita Syria:

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya chakula, afya, nyuma, maji , usafi na mauaji na utesaji Alhamisi wamezitaka pande zote zinazohasimiana katika vita vya Syria kukoma mara moja kutumia madhila ya raia kama mbinu ya vita. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Wataalamu hao wamesema wakati taarifa za mashambulizi dhidi ya raia yanaendelea , watu kutoweka kwa lazima, na mauaji ni jinamizi lingine la vita vya Syria linadhihirika, huku wakionya kuwa sasa kunyima watu huduma muhimu za maisha na kuwanyima fursa ya kupata misaada ya kibinadamu vinatumika kama mbinu ya vita.

Wameongeza kuwa kwa kuwanjima watu huduma hiozo muhimu ni kwenda kinyume na sheria za kimataifa za haki za binadamu ambazo zinamlinda kila mtu kupata huduma muhimu katika maisha.

Wataalamu wameonya kwamba vitendo hiyo ni uhalifu zidi ya ubinadamu unaotekelezwa kwa makusudi ili kuzidisha machungu kwa raia, na wamesisitiza pia ni uhalifu wa vita na ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za haki za binadamu zinazowabana pande zote wanaohusika katika vita. Umoja wa mataifa unakadiria kwamba watu milioni 9.3 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu huku wengine milioni 6.5 ni wakimbizi wa ndani. Wengine zaidi ya milioni 6 wako katika hali mbaya na wanahitaji msaada wa chakula kuendelea kuishi. Watu zaidi ya 100,000 kwa mujibu wa Umoja wa mataifa waliokwama kwenye kambi ya Yarmouk na sasa wako kwente hatari kubwa ya njaa.