Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laiomba jamii ya kimataifa iendelee kuisaidia Mali

Baraza la Usalama laiomba jamii ya kimataifa iendelee kuisaidia Mali

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limetoa wito kwa jamii ya kimataifa iendelee kuwasaidia watu na serikali ya Mali katika juhudi za kufikia amani, utulivu na maridhiano na maendeleo ya taifa hilo.

Katika taarifa ilotolewa na rais wake, wanachama wa Baraza hilo wamesema wanaendelea kutilia mkazo masikitiko yao kuhusu hali inayotia wasiwasi katika eneo la Sahel, huku wakisema wataendelea kufanya vyovyote ili kuishughulikia hali kanganishi ya changamoto za kisiasa na kiusalama, hali ambayo wamesema inahusiana moja kwa moja na masuala ya kibinadamu na maendeleo katika eneo hilo.

Baraza hilo limemwomba Katibu Mkuu kuhakikisha kuwa hatua zinapigwa mapema ili kutekeleza kikamilifu mkakati wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya taifa la Mali.