Mkutano huu ni lazima utoe matumaini ya hatma ya Syria:OIC

22 Januari 2014

Jumuiya ya nchi za Kiislam OIC ambayo inahudhuria mkutano kuhusu Syria imesema inaamini mkutano huo ni lazima uumalize machafuko yanayoendelea Syria  Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

OIC imeongeza kuwa mkutano wa leo ni lazima uhakikisha Syria inajikita katika mustakhbali wenye matumaini, uhuru, usawa, na kuheshimu haki za binadamu kwa Wasyria wote bila ubaguzi kwa misingi ya kidini, kikabila, au madhehebu ya kidini.

Akizungumza kwa niaba ya OIC katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Iyad Ameen Madan amese kuna mambo sita ya muhimu ya kuzingatia kufikia lengo hilo ambayo yaliainishwa kwenye mkutano wa kwanza wa Geneva ikiwemo kuutaka mkutano wa sasa kutekeleza yaliyokubaliwa awali kuweka muda maalumu kwa pande husika kutimiza malengo,kuwepo na ari ya kimataifa kuisaidia Syria, azimio maalumu la baraza la usalama ambalo lazima lizingatiwe na pia wao kama OIC wako tayari kubeba jukumu lolote watakalopewa

(SAUTI YA LYAD AMEEN MADAN)

“OIC pia iko tayari na ina nia ya kutumia uwezo wake wote kutekeleza jukumu lolote itakalopewa au wajibu wowote ambao utasaidia kurejesha usalama na utulivu Syria.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter