Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatafuta kambi zaidi Afrika Mashariki kwa wakimbizi wa sudani Kusini

UNHCR yatafuta kambi zaidi Afrika Mashariki kwa wakimbizi wa sudani Kusini

Idadi ya wakimbizi wa Sudani Kusini wanaovuka mpaka kuelekea nchi jirani inatarajiwa kufikia laki moja mwishoni mw amwezi January kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbiozi UNHCR.Taarifa zadi na Joseph Msami

 (TAARIFA YA MSAMI)

Tangu katikati ya mwezi December mgogoro nchini humo ulipoanza zaidi ya raia elfu 86 wa Sudani Kusini wamevuka kutafuta hifadhi nchiniUganda,EthiopianaKenyahuku UNHCR ikihaha kuanzisha kambi nyingine za wakimbizi na kupanua zilizopo ilikukidhi mahitaji yanyoonekana kukuwa kufautia mapigano ya kikabila kuendelea katika taifahilochanga.

Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

 “ Kwa mujibu wa takwimu za serikalikuna wakimbizi wa Sudani Kusini elfu 46, 579 nchini Uganda. Hadi sasa Ethipia imepokea 20,624 na Kenya takribani 8, 900. Wengine wanaokadiriwa kuwa 10,000 wamevuka kuelekea majimbo ya Sudan Kusini na jimbo la Korodofan Magharibi amabpo napo kuna mapigano. Serkali ya Sudna imesajili  1,371 miongoni mwao huku wengine wakihamahama. Maji ndio changamoto kubw aya dharura, ambapo wakimbizi waliohama hivikaribuni wamearifu kwamba inawachukua hadi siku nne kupata maji huku wengine wanalala kwenye foleni za maji na madumu yao mikononi.Malazi na afya pia ni tatizo kwani wengi wao hulala sehemu za wazi. Wengi wa wakimbizi wana umri chiniya miak 18 na wengi wao wanaulizia fursa za elimu ya sekondari na elimu ya juu. Kwa watoto waliotengana na familia zao UNHCR inatoa malazi yap eke yao na kuwatafutia walezi miongoni mwa jamii lakini msaada zaidi unahitajika  .”

 UNHCR kwa sasa inahitaji dola milioni 88 ili kutoa misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Sudani Kusini  ndani na nje ya ukanda huo.