unyanyasaji wa watoto kingono katika kanisa usio wa haki: VATICAN:

16 Januari 2014

Uongozi waVatican umekuwa ukitetea jinsi unavyoshughulikia kashifa ya unyanyasaji wa watoto kingono unaofanywa na Mapadri wa kanisa Katoliki mbele ya kamati ya Umoja wa mataifa ya haki za mtoto, CRC. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Mwakilishi wa Vatican Geneva Askofu mkuu Silvano Tomasi ameiambia kamati kwamba kanisa Katoliki inapinga jaribio lolote la maafisa wa kanisa kutaka kufunika uchunguzi unaohusisha kashifa ya unyanyasaji wa watoto kingono unaofanywa na viongozi wa dini.

Askofu mkuu Tomasi amesema unyanyasaji wa watoto kingono katika kanisa ni kosa la jinai ambalo kamwe hauwezi kuhalalishwa, akiongeza kuwa makosakamahayo ni lazima yachukuliwe hatua katika nchi yalikotendeka.

Ameongeza kuwa Papa Francis alitangaza kuanzishwa kwa tume kwa ajili ya kuwalinda watoto , ili kupambana na unyanyasaji wa kingono kwa watoto katika kanisa Katoliki na kutoa msaada kwa waathirika.

Askofu Scicluna ni mmoja wa wajumbe waVaticanwalijitokeza mbele ya kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za mtoto.

(SAUTI YA ASKOFU SCICLUNA)

"Wakati makanisa, maaskofu, au waumini wa ngazi za juu wanakabiliwa na ripoti za kashifa za unyanyasaji wa kingono wa watoto unaofanywa na viongozi wa kidini , ni lazima wafanye uchunguzi. Watoe taarifa kwausharika kwa ajili ya mafundisho ya imani, lakini utaratibu huu sio mbadala na wala hauzibi pengo la jukumu la sheria za nchi ambapo unyanyasaji wa kingono wa watoto unachukuliwa kama uhalifu mkubwa.Mataifa ambayo yanajulikana kuzuia haki , yanahitaji kuchukua hatua dhidi ya raia wan chi hiyo wanaozuia haki kutendeka kwa makosa kama unyanyasaji wa watoto kingono bila kujali watu hao ni kina nani. Sio sera ya kitakatibu kuchagiza kufunika uhalifu”

Vatican inasema inawachagiza viongozi wake wa kidini kuwasikiliza wahanga wa unyanyasaji wa kingono , kutambua machungu yao na kuwapa msaada wa kiroho na kisaikolojia kwa mtazamo wa uponyaji, upatanishi na ukarabati wa kijamii.