Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndege ya Monusco yapata ajali Goma

Ndege ya Monusco yapata ajali Goma

Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC umethibitisha kuanguka kwa ndege yake isiyo na rubani katika uwanja wa kimataifa wa Goma.

Msemaji wa MONUSCO Kanali Felix Bass amesema licha ya kuharibika vibaya kwa ndege hiyo lakini haikusababisha madhara yoyote kwa binadamu.

Kutoka huko Goma Desire Kanyama wa radio washirika Okapi ametutumia sauti ya shuhuda wa ajali hiyo