Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bunge la Uganda laridhia uwepo wa UPDF Sudan Kusini

Bunge la Uganda laridhia uwepo wa UPDF Sudan Kusini

Bunge laUganda limeridhia uwepo wa jeshi la serikali yaUgandakatika nchi jirani ya Sudan Kusini inaayokumbana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, ikiwa ni wiki kadhaa baada ya shutuma dhidi ya uamuzi wa RaisYoweri Museveni kupeleka majeshi bila ridhaa ya bunge. Hatua hiyo inakuja wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni likitoa taarifa inayokataa mzozo wa Sudan Kusini kuingiliwa na nguvu za kijeshi za kigeni. John Kibego wa Radio washirika Spice FM Uganda na ripoti kamili.

(Tarifa ya John Kibego)

Katiba yaUgandahaikubali wanajeshi kupelekwa nje ya nchi bila idhini ya Bunge. Lakini kipengele 39 cha sheria ya kuunda jeshi la UPDF kinatoa fursa kwa raisi kutuma majeshi hayo katika hali ya dharura, na kuliarifu bunge katika kipindi cha siku 21. Rais Museveni alituma majeshi hayo siku moja baada ya mapigano kuzuka Sudan Kusini.

Dakika chache baada ya bunge kuelezwa na kuuunga mkono katika kikao maalumu, Waziri wa Ulinzi Crispus Kiyonga aliongea na wandishi wa habari kuhusu udharura wa kupeleka majeshi hayo Sudan Kusini

(Sauti ya Crispus Kiyonga) 

Kwa sasa, operesheni za jeshi la UPDF Sudani Kusini, zimekubaliwa rasmi na serikali.