Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasaidia mafunzo ya polisi magereza nchini Somalia

UM wasaidia mafunzo ya polisi magereza nchini Somalia

Mafunzo ya siku tatu kwa ajili ya polisi nchiniSomalia  yanaendelea mjiniMogadishuchini ya usaidizi wa ofisi ya umoja wa mataifa nchini humo UNSOM na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC. Washiriki ni polisi wanaohusika na uangalizi wa wafungwa magerezani na wale wanaoshikiliwa rumande.

Taarifa ya UNSOM inasema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kuimarisha stadi za watendaji wa magereza nchini humo ili zikidhi viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

Mkuu wa kitengo cha pamoja cha haki na mafunzo ndani ya UNSOM Mitch Dufresne amesisitiza azma ya Umoja wa MAtaifa ya kuimarisha stadi za maafisa wa magereza nchiniSomaliaili wanapotekeleza majukumuyaoya kila siku wazingatie maadili.