Hali ya usalama huko Bor, Juba Sudan Kusini bado ni tete

Hali ya usalama huko Bor, Juba Sudan Kusini bado ni tete

Hali bado si shwari kwenye eneo la Bor, jimbo la Unity nchini Sudan Kusini, ni kauli ya Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York. Amesema kusini mwa mji huo mapigano makali yameripotiwa kati ya majeshi ya serikali na yale ya upinzani ambapo makazi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS yamezidiwa uwezo hususan katika kutoa usaidizi kwa wakimbizi wa ndani.

 (Sauti ya Farhan)

 Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaendelea kupatia hifadhi karibu watu Elfu Tisa kwenye ofisi zake huko Bor. Kazi ya kusambaza vifaa kwenye vituo vya UNMISS huko Bor sasa imekuwa ni tatiz, utoaji wa huduma za afya umezidiwa uwezo. UNMISS imeomba pande zote kutoa ushirikiano na kuruhusu ndege zinazosafirisha vifaa ziweze  kufanya hivyo.”

Nako huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini hali si shwari ambapo Farhan amesema Jumamosi usiku mapigano makali yalitokea karibu na makao makuu ya ofisi za usalama wa Taifa na kusababisha watu Elfu Moja zaidi kukimbilia kwenye ofisi za UNMISS.