Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takriban nusu ya watu wote CAR wanahitaji msaada wa kibinadamu: Feltman

Takriban nusu ya watu wote CAR wanahitaji msaada wa kibinadamu: Feltman

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Hali katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imezorota kwa kiasi kikubwa huku takriban watu milioni 2.2 wakihitaji misaada ya kibinadamu, amesema Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman, wakati akilihutubia Baraza la Usalama. Bwana Feltman amesema idadi hiyo ni karibu nusu ya idadi nzima ya watu nchini humo, huku nusu ya watu wote mjini Bangui- yaani watu 513,000- wakiwa wamelazimika kuhama makwao.

Halikadhalika, watu 750 wamethibitishwa kuuawa mjini Bangui pekee, huku idadi ya vifo nje ya mji huo ikikadiriwa kuwa kubwa. Amesema mauaji nchini humo yanaendeshwa kila siku, huku watu wakiwa wamegawika kwenye misingi ya kidini na kuweka vituo vya ukaguzi vinavyosimamiwa na watu ambao ama wanaegemea upande wa dini ya Kiislamu au dini ya Kikristo.

Bwana Feltman amesema wanawake na watoto ndio walioathirika zaidi na machafuko ya CAR, huku akitoa wito machafuko na uhalifu dhidi ya raia kukomeshwa.

“Walio kwenye nafasi za mamlaka au ushawishi ni lazima wafanye wawezalo kusitisha machafuko na kusitisha uhalifu mkubwa unaotekelezwa dhidi ya raia, wakiwemo watoto. Mashambulizi dhidi ya watoaji huduma za kibinadamu na matumizi ya vituo vya umma kama shule na hospitali kwa shughuli za kijeshi ni lazima pia yakomeshwe. Nimeliomba Baraza kukukmbusha tena wahusika katika mzozo kuhusu wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu, na kuhakikisha kuwa wote wanatenda uhalifu wanawajibishwa kisheria.”

Bwana Feltman amesema kuna hofu kuwa machafuko hayo huenda yakavuka mipaka na kuathiri usalama na utulivu kwenye ukanda mzima, akiongeza kuwa ni wajibu wa wote kuchukuwa hatua sasa kuepusha majuto.