Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waziri mkuu wa Somalia akutana na mwakilishi wa UM

Waziri mkuu wa Somalia akutana na mwakilishi wa UM

Waziri mkuu mpya wa Somalia amekutana kwa mara ya kwanza na mwakilishi wa Umoja wa mataifa nchini humo Nicholas Kay mwishoni mwa wiki tangu aliposhika wadhifa huo.

Waziri Abdiweli Sheikh Ahmed amemshukuru Bwana Kay kwa Umoja wa mataifa kuendelea kusaidia ujenzi mpya wa Somalia na anatarajia kuendelea kuwepo kwa ushirikiano mzuri katika siku za usoni.

Kwa upande wake Kay amempongeza waziri Ahmed kwa kuteuliwa kwake na wawili hao wakajadili kuhusu kuundwa kwa baraza jipya la mawaziri, mkakati wa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2016 na msaada wa kimataifa kwa Somalia kupitia muafaka mpya.

Pia wamejadili suala la kupanua wigo wa operesheni za usalama dhidi ya wapiganaji wa Al shabaab baada ya baraza la usalama kuidhinisha uongezaji wa vikosi vya AMISOM na misaada ya kiufundi.