Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yatoa wito kwa jamii za Sudan Kusini kudumisha utengamano

UNESCO yatoa wito kwa jamii za Sudan Kusini kudumisha utengamano

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, ametoa wito wa kwa jamii za Sudan Kusini kuheshimu minyambuliko ya kijamii, huku akielezea masikitiko makubwa kufuatia kuongezeka kwa machafuko nchini humo. Assumpta Massoi na taarifa kamili

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Bi Bokova amelaani kuuawa kwa watu na kuongezeka uhasama miongoni mwa jamii tofauti, na kuzihimiza pande zote husika kuheshimu tofauti za kitamaduni za nchi hiyo. Amesema kuheshimu utofauti wa kitamaduni ni suala kimaadili, kama ilivyo kuheshimu haki za binadamu.

Ameongeza kuwa kudumisha amani kunahitaji kujitoa kwa mazungumzo kama njia pekee ya kuimarisha utangamano baina ya watu na jamii, huku akitoa wito hususan kwa vijana wa Sudan Kusini kuwa kielelezo cha mabadiliko na maendeleo ya taifa lao jipya, kwa kutatua mizozo ya kisiasa kwa njia ya amani.

Bi Bokova pia amesema kwa kuwa elimu ni kitu cha kuaziziwa katika kuweka maendeleo na amani endelevu, shule na taasisi za elimu zinatakiwa zilindwe na kuheshimiwa kwa mchango zinazotoa kama mahali pa kujenga amani katika akili za watu na maendeleo.