Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale: Majanga na Ustawi

Hapa na Pale: Majanga na Ustawi

Majanga ya kiasili na yale yasababishwayo na binadamu yalitikisa mwaka 2013, Kimbunga Haiyan kilipiga Ufilipino na kuua zaidi ya watu Elfu Sita na mamilioni kupoteza makazi na hata uharibifu wamali!

Ukanda wa Sahel huko Mali, mapigano, mabadiliko ya tabianchi yalishika kasi, lakini kote Umoja wa Mataifa ulijitokeza na kuonyesha mshikamano na wakazi wa eneo hilo kwa kuibuka na mkakati wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi na matumaini kuanza kurejea. Jamhuri ya Afrika ya Kati, hali bado si shwari, lakini Umoja wa Mataifa unang’ang’ana kuleta matumani siyo tu mji mkuu Bangui bali pia na viungani.