Baraza Kuu lamkumbuka Nelson Mandela

19 Disemba 2013

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao maalumu cha kumkumbuka Hayati Nelson Mandela, siku chache baada ya kuzikwa kwake siku ya Jumapili. Joshua Mmali na taarifa kamili

(TAARIFA YA JOSHUA)

Tumekusanyika hapa leo kumuenzi mtu ambaye si wa kawaida, Nelson Mandela. Mtu ambaye alitoa msukumo kwa taifa lake, bara na ulimwengu mzima kupitia vitendo vyake na mawazo yake. Mtu kama huyo hawezi kusahaulika, siyo nasi tuliokusanyika hapa kumuenzi, watoto wetu na hata wajukuu wetu.”

Ni rais wa Baraza Kuu, John William Ashe, katika kikao hicho maalumu kilichoanza kwa nyimbo, na kufuatia na hotuba za kumsifu Mandela. Miongoni mwa waloongea ni Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, ambaye amekumbuka halaiki ya watu walojitokeza kumuenzi Hayati Mandela kwenye ibaada zilizofanywa kabla ya mazishi yake.

Balozi Kingsley Mamabolo, Mwakilishi wa Kudumu wa Afrika Kusini, amelishukuru Baraza Kuu kwa kuandaa kikao cha leo, na ulimwengu mzima kwa jinsi ulivyoonyesha upendo kwa Mandela

Kwa wakati huu, ilidhihirika kwetu kuwa, kifo cha Madiba kimetugusa sote, kote duniani. Tumefarijiwa na ujumbe wenu wa rambi rambi. Raia wa Afrika Kusini wanaweza kuliwazwa na jinsi kifo cha Mandela kilivyowaleta pamoja.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud