Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa UM aitaka Malaysia kutowatenga maskini

Mtaalam wa UM aitaka Malaysia kutowatenga maskini

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za chakula Olivier De Schutter amesema kuwa wakati taifa la Malysia likipiga hatua kuwa taifa lenye kipato cha juu, linapaswa kuhakikisha kwamba mafanikio hayo hayapatikani kwa mgongo wa uharibifu wa mazingira wala mgongo wa makundi ya watu wenye hali ngumu.

Akiwa kwenye kilele cha ziara yake nchini humu mtaalamu huyo amesema kuwa Malaysia inapaswa kuangalia namna inavyoendesha shughuli zake za kimaendeleo pasipo kuathiri maeneo mengine.

Lakini hata hivyo ametambua mchango mkubwa unatolewa na taifa hilo akisema kuwa katika kipindi cha miaka michache iliyopita, Malaysia imepiga hatua kwenye maeneo ya maendeleo na tija kwa wananchi wake.

Amesema changamoto kubwa iliyosalia mbele ni kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakabili kizazi cha pili