Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wanachangia katika kupunguza umaskini: Umoja wa Mataifa

Wahamiaji wanachangia katika kupunguza umaskini: Umoja wa Mataifa

Leo ni siku ya kimataifa ya wahamiaji ambapo Umoja wa Mataifa unataka mazingira bora zaidi kwa watu Milioni 232 waliohama makwao na kwenda ugenini kwa sababu mbali mbali ikiwemo kusaka maisha bora.  Joshua Mmali na ripoti kamili.

(Ripoti ya Joshua)

Uhamiaji wa kimataifa ni njia thabiti ya kupunguza umaskini na kuongeza fursa, na ni jambo asilia kwenye karne hii ya 21, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika ujumbe wake kwa siku hii. Amesemahiloni dhahiri kwani kazi zinazofanywa na wahamiaji zinaboresha maisha kule walikohamia na hata walikotoka. Hata hivyo Bwana Ban amesema katika kusaka maisha bora wahamiaji wasio na stadi za kutosha wanakumbana na mkwamo katika kujiendeleza kwenye jamii wanamoishi na wakati mwingine hutumbukia katika maisha yasiyo na staha. Ametaka serikali kuzingatia sheria ikiwemo kuepusha chuki dhidi ya wahamiaji, manyanyaso na hata vikwazo. Haji Hamis ni mtanzania aliyehamia Marekani miaka 13 iliyopita, anazungumziaje mazingira ya ughaibuni.

(Sauti ya Haji Hamis)

Wakati huo huo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John William Ashe amesema mwaka 2013 uliweka historia katika mewl ekeo wa maisha bora ya wahamiaji kwa kujumuisha sualahilokwenye ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Amesema hakuna kurudi nyuma na uhamiaji si jambo la kupigwa marufuku, bali linataka usimamizi bora.