Msaada wa dharura wa chakula wawafikia wahitaji CAR:WFP

10 Disemba 2013

Tathimini ya pamoja nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imebaini kwamba ghasia zilizozuka upya Desemba 5 mwaka huu zimewatawanya watu zaidi ya 60,000 na chakula ni suala lililo msitari wa mbele kwao.

 Na kwa kutambua hilokatika kukabiliana na mahitaji muhimu ya haraka shirika wa mpango wa chakula WFP linatoa msaada kwa waathirika kwenye mji mkuuBanguipamoja na Bossangoa Kaskazini  Magharibi mwa nchi.

 Kwa mujibu wa naibu mkurugenzi wa WFP nchini humo Guy Adoua hali ya kibinadamu nchini humo ni mbaya na itazidi kuzorota wakati watu wakiendelea kuathirika na vita. WFP na washirika wake wanahitaji kuwa msitari wa mbele kutoa msaada na kusaidia wale wasiojiweza ameongeza Adoua.

 Hata hivyo amesema licha ya matatizo ya kiusalama WFP imeshatoa msaada wa chakula kwa watu zaidi ya 19,000 mjiniBanguikatika siku tatu za mwanzo wa machafuko, huku huko Bossangoa ugawaji chakula ulitiwa dosari na ghasia kwa siku nne lakini sasa umeanza tena.