Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwezi mmoja baada ya Haiyan, afya ya uzazi bado mashakani Ufilipino: UNFPA

Mwezi mmoja baada ya Haiyan, afya ya uzazi bado mashakani Ufilipino: UNFPA

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu, UNFPA limesema mwezi mmoja baada ya kimbunga Haiyan kupiga Ufilipino, bado afya ya wajawazito na watoto wanaozaliwa iko mashakani na hivyo linaomba usaidizi zaidi kwa watu Milioni Tatu nuktaSabaambao ni wanawake na wasichana walio kwenye umri wa kubeba ujauzito. Shirikahilolinasema kila siku kwenye maeneo yaliyopigwa kimbunga wajawazito 900 hujifungua katika mazingira duni, ikiwemo majumbani na idadi hiyo yatarajiwa kuongezeka. Imesema katika hospitali  ya Capiz, wajawazito wawili walifariki dunia baada ya kukosa damu ya kuongezewa. Mwakilishi wa UNFPA nchini Ufilipino Genevieve Ah Sue amesema wanawake na wasichana wanabeba janga la kimbunga na kwamba usaidizi unaoelekezwa kwa makundi hayo utaweza kuwahakikisha afya, usalama na ustawi wa familia zao. UNFPA inahitaji zaidi ya dola Milioni 16 na nusu kwa ajili  ya kuboresha huduma za afya ya uzazi ikiwemo kukidhi mahitaji ya wanawake na wasichana kwenye manispaa 22 nchini Ufillipino.